TANUA MIPAKA YAKO ULICHO NACHO KINAWEZA KUKUSOGEZA
2 Elisha akamwambia, Nikufanyie nini? Niambie; una kitu gani nyumbani? Akasema, Mimi mjakazi wako sina kitu nyumbani, ila chupa ya mafuta.
3 Akasema, Nenda, ukatake vyombo huko nje kwa
jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usitake vichache.
4 Kisha uingie ndani, ukajifungie mlango wewe
na wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo vilivyojaa ukavitenge.
5 Basi akamwacha, akajifungia mlango yeye na
wanawe; hao wakamletea vile vyombo, na yeye akamimina.
6 Ikawa, vilipokwisha kujaa vile vyombo,
akamwambia mwanawe, Niletee tena chombo. Akamwambia, Hakuna tena chombo. Mafuta
yakakoma.
2 Waf 4
Haya mambo mawili
tuyatafakari
- Ulicho nacho kina maana sana.
Huenda usijue thamani ya
ulicho nacho hadi siku Yesu akutokee na akuulize una nini? Musa aliwai kuulizwa
na yeye una nini mkononi mwako?. Huenda una elimu ila huna kazi na kwa sababu
iyo umekata tamaa ya kuendelea kusoma degree ya pili ukifikiri elimu kwako
haina msaada wowote, wewe tulia tu kuna siku utaulizwa una nini? na iyo elimu
itakutoa mahali uliko.
Huenda pia huna elimu
kubwa hata ila unajua kidhungu, wewe tulia tu usijisikie vibaya kuona wengine
wamesoma ukafikiri huna future. Yesu akikutokea akakuuliza una nini? mwambie
nina jua kidhungu.
- Panua hema yako, enlarge your boundaries.
Huyu mama kitu alicho
ambiwa ni kuleta vyombo tena vya kuazima kwa jirani ...ndani ya nyumba yake.
Ivi umejiuliza kwa nini huu muujiza ilikua lazima utendeke ndani?. Nalijaribu
kuwaza kama huyu mama angekua na jumba kubwa kama la Rahabu yule alikua kahaba
angejaza vyombo vingi Zaidi. Kuna namna naona hapa ya kwamba Mungu hawezi
kukutendea muujiza Zaidi ya mipaka uliyo nayo. Kama umekula shule hadi form six
ujue iyo yaweza kuwa limit ya Mungu katika kukutendea baadhi ya mambo. Mungu
hawezi kukutendea muujiza mkubwa Zaidi ya mipaka yako. Biblia inasema mahali
pengine "Kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu" maana yake ni
kwamba kiwanago cha nguvu uliyo nayo inawezekana ikawa limit ya Mungu kufanya
kwako.
Kuna mtumishi mmoja
sitokuja nimsahau maishani mwangu anaitwa Yebesi. Huyu ndugu akiwa katika
maombi yake alimwambia Mungu ambariki kisha atanue mipaka yake. Alijua kabisa
Baraka za Mungu zinaweza kuwa limited na mipaka aliyo nayo. Mipaka yako huenda
ndio iliyo fanya uwe na hali ya maisha uliyo nayo sasa na sio kwamba kuna mtu
kakuloga.
10 Huyo Yabesi
akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na
kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda
na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba
1 Nyak 4
1 Chronicles
4:10Amplified Bible (AMP)
10 Jabez cried out
to the God of Israel, saying, “Oh that You would indeed bless me and enlarge my
border [property], and that Your hand would be with me, and You would keep me
from evil so that it does not hurt me!” And God granted his request.