Header Ads

JE UNA NINI MKONONI MWAKO? - Part 1

Kut 4:1-3
Musa akajibu akasema, Lakini, tazama, hawataniamini, wala hawataisikia sauti yangu; maana watasema, Bwana hakukutokea.. Bwana akamwambia, Ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako? Akasema, Ni fimbo. Akamwambia, Itupe chini; akaitupa chini, nayo ikawa nyoka; Musa akakimbia mbele yake.
Mambo unayopaswa kujiuliza baada ya kusoma hapo juu
1.       Je ulichonacho kimekupa ujasiri wa kusonga mbele?
2.       Ulichonacho kinakuongezea uwezo wa kujiamini?
3.       Nini kinafanya usijiamini pamoja na kujua ulicho nacho?
4.       Je unajua thamani ya ulicho nacho?
5.       Je unajua kwanza una kitu gani?
6.       Je unajua kitu ulicho nacho kikitumika ipasavyo kinamtambulisha Mungu uliye nae?
7.       Je umewakithamini kitu ulicho nacho?
8.       Thamani ya ulicho nacho iko kwa nani?
Utangulizi
Musa hakufahamu kabisa kwamba watu kumuamini na kumsikiliza kunategemea na alicho nacho. Watu kuamini kwamba ana Mungu kulikua kunategemea na matumizi ya kile alicho nacho. 

Pamoja na kuwa na fimbo mkononi mwake lakini Musa hakujua thamani ya ile fimbo. 

Thamani ya fimbo aliyokua nayo Musa ilikua imejificha kwa Mungu. Mwenye kuitambulisha thamani ya ulicho nacho ni Mungu peke ake.
Ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako? Hii ilitaka tuone Mungu ameweka kitu juu ya mtu na hiko alichokiweka ana matumizi nacho. Tuangalie mifano kadhaa hapa chini:-
Mfano wa kwanza: - Daudi
49 Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi.
1 Sam 17
Klichomfanya Daudi ajulikane kitaifa na kimataifa ni Jiwe alilokua nalo mkononi. Umefikiri kitu ulichonacho kinaweza kubadilisha tafasili nzima ya maisha yako kwa kiwango hiki. Kitu kingine kilichompa ujasiri Daudi ni kwamba alilipa thamani jiwe alilokua amebeba. Wako watu wanadharau vile walivyo navyo wakiamini haviwezi kuwasaidia.
Mfano wa Pili: - Jaribu la Yesu
Yoh 6:4-9
Na Pasaka, sikukuu ya Wayahudi, ilikuwa karibu. Basi Yesu alipoinua macho yake akaona mkutano mkuu wanakuja kwake, alimwambia Filipo, Tununue wapi mikate, ili hawa wapate kula? Na hilo alilinena ili kumjaribu; kwa maana alijua mwenyewe atakalotenda. Filipo akamjibu, Mikate ya dinari mia mbili haiwatoshi, kila mmoja apate kidogo tu. Wanafunzi wake mmojawapo, Andrea, nduguye Simoni Petro, akamwambia, Yupo hapa mtoto, yuna mikate mitano ya shayiri na samaki wawili, lakini hivi ni nini kwa watu wengi kama hawa?”
Ambacho Yesu alitaka kufanya sio tu kuwatendea muujiza ila kuwapa shule ya juu ya thamani ya kitu ulicho nacho ukikitumia kwa kumtazama Mungu. Ile mikate kimsingi haikuwa kwenye mikono ya Yesu ila mikononi mwa mtu asiye jua namna ya kukitumia. Unachopaswa kuelewa ni kwamba ulicho nacho unapaswa kumruhusu Mungu akaitumie kubadilisha thamani yake.
Ukifuatilia utafikiri kama Filipo hakua hata msomaji wa maandiko kama ingekua yuko leo. Kwa sababu unaweza kujiuliza kama Filipo alikua anasoma biblia (ingekuwepo wakati huo) angeweza kusema Mungu mie ninajua kwamba jangwani akina Musa uliwalisha Mana, basi tumia pia huu mkate kutulisha na sisi wote. Lakini huyu bwana sijui kwanini hakuchomokea toka kwenye zaburi ya 23 alipoulizwa juu ya ile mikate.

Unaposoma maandiko hakikisha yanalisha kitu ulicho nacho, hakikisha unasoma biblia kwa jicho la kubadili maisha yako. Wengi wanasoma biblia ili wakahubirie watu wengine ila sio kulisha walivyo navyo ndani yao. Sina maana kwamba usisome ili uhubirie watu ila hakikisha ukisoma neno linalisha na ndoto yako. Hasara moja wapo unaweza kuipata ukisoma biblia bila kujijua wewe ni nani ni kushindwa kuitumia biblia kulisha ndoto yako.

Mfano wa Tatu:- Yusufu alikua na uwezo wa kutambua ndoto
Kilichompandisha chati Yusufu sio tu ndoto aliyoota isipokua ni uwezo aliokuwa nao ndani ya moyo wake wa kutafasili ndoto. Utafasili wa ndoto ndio uliomfanya kutambulika hadi katika nchi ya ugeni. Mungu aliitumia uwezo alikua nao Yusufu juu ya kutafasili ndoto kubadilisha kiwango cha maisha yake.
ITAENDELEA.......
Theme images by centauria. Powered by Blogger.