Header Ads

JE UNA NINI MKONONI MWAKO? - Part 2

KUTOKUJUA UNA NINI HAKUMZUII MUNGU KUKUTUMIA
 

Musa
Hakikumsumbua Mungu kumtumia Musa japo hakuwa amejua fimbo aliyo nayo ina maana tosha katika kuutekeleza wito aliopewa. Kama ungebahatika kukutana na Musa na kumuuliza kwa nini likua ameshika fimbo huenda angekujibu amezoe kwa sababu alikua mchungaji wa wanyama.
Yeremia
Mungu alikua ameweka kitu kwenye macho ya Yeremia wakati anamuumba. Hiko kitu kwenye macho yake ndicho kilichomtofautisha na watu wengine. Sasa Yeremia kutokujua maana ya anachoweza kukiona kwa macho yake haikumzuia Mungu kutokumtumia. Jaribu kufikiri nini kilimsukuma Mungu alipomtokea Yeremia gafla akaenda moja kwa moja kwenye macho yake?. Mungu alijua kabisa kinachoweza kumtofautisha Yeremia kwenye utumishi alio weka ndani yake ni kile ameweka kwenye macho yake. Don’t under estimate what you have hata kama hujui kimebeba nini. Kaa na Mungu, kipambanishe hiko ulicho nacho na Neno la Mungu kitafunuliwa kwako ukakielewa.
Petro
Math 4:18-19
‘Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi. Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu”
Petro hakujua uvuvi uliowekwa ndani yake una manufaa gani kwenye hatima ya maisha yake lakini ilo swala halikumzuia Yesu kuwatumia. Yesu atakufata tu hata kama hujui una nini na kinahitajika saa ngapi. Akija kwako uwe na uhakika kwanza atafanya ujue thamani ya ulicho nacho kisha akuruhusu ukifanyie kazi ulicho nacho. Uhusiano ulionao wewe na Yesu ndio utakao fanya ugundue uthamani wa ulicho nacho.
Kilichomfanya Daudi ajue kwamba jiwe alilo nalo mkononi thamani yake ni kubwa kuliko silaha kali za vita ni ule uhusiano aliokua nao na Mungu.


MAMBO YA KUKUMBUKA
Unaweza kujua ulicho nacho lakini kikaibuka kitu kingine kukukwamisha. Ukifatilia mazungumzo ya Mungu na Yeremia utagundua tatizo pekee kwa Yeremia halikua kukataa wito isipokua kufikiri umri wake bado hautoshi kufanya anachokiona. 

Kilichomsukuma Mungu kumwambia usiogope ni kutokana na kwamba umri uliingiza hofu ndani ya moyo wa Yeremia. Inawezekana kabisa una kitu kikubwa ndani yako cha kubadili huu ulimwengu lakini na wewe unafikiri umri ulio nao bado hautoshi. Sikia neno la Bwana “inuka anza kuitenda iyo kazi Mungu yuko pamoja nawe kuitenda”.
Mazingira hayakumfanya Yusufu kuacha kutumia uwezo wake wa kutafasili ndoto. Shetani anaweza kukuingiza kwenye mazingira ambayo lengo lake kuvuruga mind set yako ukaacha kupalilia kile ulicho nacho na kuanza kulalamikia mazingira. 

Yusufu angeweza kung’ang’ana na malalamiko kwamba hakustahili kuwa gerezani lakini iyo mbinu ya shetani haikufanikiwa. Kama upo kwenye mazingira unaishi na unafikiri huyapendi yasikufanye ukaacha kutumia kile Mungu ameweka ndani ya moyo wako. 

Huwezi jua Mungu atakutembelea kwa wakati gani. Kilichomtambulisha Mungu wa Yusufu kwenye ile nchi ya ugeni ni kile Mungu aliweka ndani ya Yusufu. Kutotumia ulichowekewa ndani yako kuna hatari ya kutomfanya Mungu atambulike hapo ulipo. Kati ya shauku unapaswa kuwa nayo unapokitumia kile Mungu ameweka ndani yako ni ili yeye atukuzwe kwa wale watako kusikia au kukuona.
  
UNAJUAJE KITU ULICHO NACHO

Angalia kitu gani unapenda kufanya Zaidi kisha muulize Mungu kutokea hapo. Wakati unaendelea kumuuliza Mungu hakiksha unasoma neno kila wakati ili Mungu akisema nawe upate kuelewa. 

Huwezi kupata majibu kwa nini Musa alikua na fimbo, ndivyo ambavyo unaweza usiwe na majibu kwa nini unapenda kuwa na hiko ulicho nacho. Hivyo muombe sana Mungu taratibu akueleze nini ameweka ndani ya moyo wako. Hakuna swali lolote utakalo kwenda nalo kwa Mungu asilijibu ikiwa umeomba ndani ya mapenzi yake.


13 Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. 14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. - Yohana 14


Theme images by centauria. Powered by Blogger.