Header Ads

BWANA MUNGU WAKO ANATAKA NINI KWAKO KABLA YA KUMTUMIKIA?


“Na sasa, Israel BWANA MUNGU wako anataka nini kwako, ila umche BWANA, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote na kumpenda na kumtumikia BWANA MUNGU wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote.” Kumb 10:12
Sio watu wengi sana wanafuatilia hili swali kabla ya kuanza kumtumikia Mungu katika maisha yao kwa nafasi Mungu alizowapa. Mambo anayotaka uyafatilie ni;-
1.      Umche
2.      Kwenda katika njia zake zote
3.      Kumpenda
Baada ya mambo haya matatu ndipo Mungu anaachilia nafasi ndani ya mtu kwa ajiri ya yeye kuitwa mtumishi wake.
Unaweza kutumika mahali lakini mbingu haina kumbukumbu zako ya kwamba wewe ni mtumishi wa Mungu pamoja na kwamba unatumika kanisani na umeokoka vizuri kabisa. Ndio sababu ukiendelea mbele Mungu anasisitiza umtumikie yeye. Unapaswa kuelewa hadi kuna msisitizo wa kumtumia yeye kuna wengine basi unaweza kuwatumikia ukafikili unamtumikia yeye.
Kumb 10:20
“Mche BWANA MUNGU wako, umtumikie yeye, ambatana naye na kuapa kwa jina lake.”
Isikusumbue kwa sababu unatumika kanisani ukajipa uhakika unamtumikia Mungu, ni vizuri kufuatilia hatua alizioweka nyuma kabla ya utumishi. Wako watu wanatumika vizuri kanisani lakini si watumishi wa Mungu.
Mfano : Kwa Yoshua, Yosh 1:1
“Ikawa baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa BWANA, BWANA akamwambia Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa , akasema……..”
Ndugu Yoshua yote aliyokuwa akifanya hapo nyuma biblia inatupa kujua alifanyika mtumishi nyuma ya Musa. Nafasi ya utumishi ilikuwa sasa halisi kama mtumishi wa Mungu kwa sababu huyu ndugu alifatilia yale mambo ya msingi matatu.
Ukiendelea kusoma mistari ya hapo utaelewa na mimi ya kwamba hapo kabla kama alikuwa anamsikia Mungu si katika kiwango kile alichokua nacho Musa, ndio sababu Mungu anampa uhakika ya kwamba nitakuwa na wewe katika kiwango kile kile nilichokuwa na Musa bila hata kukupungukia.
Yosh 1:5
“…….kama niliyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe, sitakupungukia wala kukuacha…..”
Nisingekuuliza swali hili nililokuuliza ulipaswa kujiuliza swali la hivi “ Bwana Mungu anataka nini kwako?” hii ni kutokana na kitabu tulichokisoma cha kumbukumbu la Torati. Ukijiuliza hili swala la Bwana Mungu anataka nini kwako unatakiwa kujua mambo yafuatayo:-
1.      Umche yeye
2.      Kwenda katika njia zake zote
3.      Kumpenda
4.      Kumtumikia kwa moyo wako wote na roho yako yote
5.      Kuzishika amri zake alizokuamuru
Baada ya kuangalia haya mambo matatu Mungu anakuhakikishia ya kwamba mbingu ni mali zake ,mbingu za mbingu, na nchi na vitu vyote vilivyomo. Maana yake ni kwamba anakupa uhakika wa kutokuwa masikini na kuangaika na maisha kwa namna yoyote ile baada ya kuyaangalia hayo mambo matano.
Sasa mimi nimeweka haya mambo matatu kabla ya utumishi kwa sababu nasikia msukumo wa kukupatia maelekezo ya kutosha kukusaidia katika utumishi ulio mbele yako. maana biblia inasema si wote waitao Bwana Bwana watauona ufalme wake.
Math 7:17-23
“Si kila mtu aniambiaye ,Bwana Bwana atakaye ingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile Bwana………”
Hapa ndugu Matayo anajaribu kuzungumza na watumishi ambao wajazingatia yale mambo matatu nimekueleza hapo juu. Na ninapokufundisha haya ninataka utoke katika kundi la watumishi watakao lalamika huko mbinguni.
Lakini si hayo mambo matano tu Mungu anahitaji toka kwako ni zaidi ya hayo, kwa mfano unapoonganisha kitabu cha kumbukumbu la torati na kitabu cha Mika utagundua Mungu anataka mambo takribani nane toka kwako.
Mika 6:8
“ Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema, BWANA anataka nini kwako ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.”
Hivyo unapata kujua mambo yafuatayo ambayo Mungu anataka kwako;
1.      Umche yeye
2.      Kwenda katika njia zake zote
3.      Kumpenda
4.      Kumtumikia kwa moyo wako wote na roho yako yote
5.      Kuzishika amri zake alizokuamuru
6.      Kutenda haki
7.      Kupenda rehema
8.      Kwenda kwa unyenyekevu na Mungu

KWENDA KATIKA NJIA ZAKE ZOTE
Unapoanza kumtumikia Mungu katika nafasi yoyote ile tunategemea kuona unafanikiwa na unasitawi sana. Chukua somo ili kama mtaji wa kujitafakari…..ASANTE
Theme images by centauria. Powered by Blogger.