UNAUTAZAMAJE UZINZI KATIKA MAISHA YAKO NA KRISTO
‘lakini mimi nawambia, kila mtu
amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini moyoni mwake.’
Math 5:28
‘Ikimbieni zinaa, Kila dhambi
aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda
dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.’ 1Kor 6:18
Uzinzi kama
uzinzi una matokeo katika mwili na roho ya mwanadamu. Lakini waliowengi
wamekuwa wakifuatilia matokeo ya uzinzi katika miili yao na mara chache katika
roho zao.
Uzinzi una
matokeo mengi kati ya hayo ni pamoja na
·
Kuingiza miungu ya mtu unayezini naye
·
Kumwagiwa uzinzi na unayezini naye
·
Kupata ukimwi na magonjwa mengine
·
Kupata mimba usiyo tarajia
Kuingiza miungu ya kigeni kwa njia ya
uzinzi
Unapofanya
uzinzi na mtu jua kwamba pia unafanya ilo tendo na miungu yake hivyo
unaikaribisha kwako.
‘…..watu wakaenda kufanya uzinzi na
miungu yao……’ Kut 34:15, 12
Kuna athari
za kuingiza miungu ya kigeni katika maisha yako mkristo. Kuingiza miungu ya
kigeni kupitia tendo la ndoa maana yake ni kufanya agano na hiyo miungu. Na
kinachotokea unapofanya agano na miungu migeni inakaa katikati yako.
Kilichomtokea Selemani mfalme
Selemani
alikaribisha miungu ya kigeni kwa njia ya tendo la ndoa
JINSI GANI UNAWEZA KUEPUKA UZINZI
Biblia
imetoa ushauri mmoja mkubwa sana wa moja kwa moja juu ya nini cha kufanya ili
kuepuka uzinzi.
Kabla
sijakwambia jinsi ya kuepuka nikukumbushe jambo hili. Uzinzi ni uzinzi pamoja
na makundi yake yote isipokua matokeo ya uzinzi ni tofauti katika muonekano
wake. Kuna watu ambao wanazini kwa mawazo lakini si kwa tendo kama wanavyosemwa
katika Mathayo
‘lakini mimi nawambia, kila mtu
amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini moyoni mwake.’ Math 5:28
Na kuna watu
ambao wanazini kwa tendo na kwa mawazo nao ni wazinizi.
Lakini
ushauri wa moja kwa moja wa kibiblia kwa makundi yote haya ni kuukimbia.
‘Ikimbieni zinaa, Kila dhambi
aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda
dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.’ 1 Kor 6:18
Unaukimbiaje uzinzi kwa njia ya
mawazo?
Uzinzi wa
kimawazo unakimbiwa kwa kuepukana na mazingira shawishi. Kwa mfano kama hutaki
uzinzi wa kimawazo usiangalie picha za wadada wakiwa watupu, picha za ngono n.k
au usikae mahali wanakozungumza stori za kuzini.
Ninakwambia
hivi kwa sababu hiki ndicho kitu kilichomsaidia Yusufu hakutaka stori na yule
mke wa mfalme.
‘Akawa akazidi kusema na Yusufu siku
baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye.’ Mwa 39:10
Kwa sababu
uzinzi wa mawazo unafanyikia moyoni kwanza kabla ya mwilini ni vizuri kuujaza
moyo neno la Mungu kiasi ambacho hakuta kuwa na nafasi ya kitu kingine. Maana
biblia inatuambia kama moyoni kumejaa neno na kiukweli unalifuata huwezi
kutenda dhambi kabisa.
‘moyoni
mwangu nimeliweka neno lako nisije Bwana nikakutenda dhambi mimi.’
Uzinzi wa mwili unakimbia vipi?
Tujifunze
kwa Yusufu tena
‘huyu mwanamke akamshika nguo
zake,akisema , Lala name. Yusufu akaiachia nguo yake mikononi mwake akakimbia,
akatoka nje’ Mwa 39:12
Nataka
uyaone haya maneno mawili
·
Akamshika
nguo zake
·
Akatoka
nje
Wako wadada/wakaka
hadi wanavuliwa nguo bado wanashangaa tu wakati Yusufu aliposhikwa tu akili
ilichange. Sasa wewe unashikwa nguo still utoki nje unategemea kitu gani
mtumishi.
Haiwezekani
kwamba hutaki uzinzi na bado unakaa chumbani na mwanaume/mwanamke unayemtamani.
Mwisho
Mwisho