NITAKUWA NI ADUI WA ADUI ZAKO, NA MTESI WA HAO WAKUTESAO
Bwana Yesu asifiwe msomaji!
Karibuni tuumege mkate wa leo.
Kutoka 23 :22
Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao.
Mstari huu unatuonesha kwa kiasi utaratibu wa Mungu katika kuwaongoza na kuwapigania wale wanao sikiliza sauti yake na kutenda maagizo ya Mungu na kuzishika amri zake
Hapo juu tunaona Mungu akiahidi kuwa Yeye atakuwa adui wa adui zetu na mtesi wa hao watutesao. Nani asiyependa kuwa na ulinzi wa Mungu?
Tukumbuke katika neema hii ya ulinzi wa Mungu, kuna sauti ya Neno lake ambalo lina maagizo mengi na ya tofauti tofauti tunayopasa kuyaskia. Miongoni mwa sauti ya Mungu anayotusikizisha tusomapo ujumbe huu ni pamoja na hii tunayoisoma katika 1 Thes 5:14
1 WATHESANIKE 5:14
Ndugu, twawasihi, waonyeni wale wasiokaa kwa utaratibu; watieni moyo walio dhaifu; watieni nguvu wanyonge; vumilieni na watu wote.
Hebu tutafakari maneno haya:-
A) Kuwaonya wasiokaa kwa utaratibu.
Hapa tunatakiwa kuitumia neema ya Kristo kuweza kuwasaidia wengine ambao bado hawajapata neema ya wokovu ili wapate kuokoka lakini pia hata wale ambao wameokoka lakini hawaendi sawasawa na maagizo ya Mungu.
B) Kuwatia moyo walio dhaifu
Najua tunajua faida za kumtia moyo mtu na sii kutumia udhaifu wa mtu kumyanyasa na kumfanya arudi nyuma. Kwa Kumtia mtu moyo utamfanya mtu huyo kutokujinyanyapaa kwa namna yoyote maana ndani yake unampa tumaini na kumfanya atambue kua hata yeye Krsto alikufa kwa ajili yake.
C) Kuwatia nguvu walio wanyonge
Kila mtu ana mapito yake, na ni muhimu kujua kuwa wengine katika majaribu na mapito yao huweza kuwadhoofisha kiroho, hivyo ni muhimu kuwatia moyo ili katika kipindi hiki wasirudi nyuma na kuiacha kweli ya Mungu.
D) Vumilieni watu wote
Kama ilivyo tunaishi na watu tofautitofauti na kila watu wanaweza kuwa na tabia zao, miiko yao na mapokeo yao, hivyo unapopata neema ya Mungu kuwahudumia ni lazima ujifunze hekima ya kuchukuliana nao iwe ni katika udhaifu au kwa namna yoyote ile, maana kwa kufanya hivyo utawafanya kukuona wa tofauti na hivyo kuwageuza nia zao na kumgeukia Mungu ktk Yesu.
Katika yote tunatakiwa tuhakikishe haturudi nyuma and we don't let any one to turn back, forward we go in Jesus' name and by the help of the Holy Spirit.
Na: Grace PinielKujiunga na darasa letu la watsap tuandikie watsap +255758358236