YEYE NDIYE ATAWAOKOA WATU WAKE NA DHAMBI ZAO
21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
Mathayo 1 :21
Bwana Yesu asifiwe!!
Tumeingia tena kipindi cha kukumbuka kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristu.
Lengo la Yesu kuzaliwa kwetu ni ili aje kutuokoa na dhambi zetu. Ninaomba tujitathmini ya kuwa mpaka tuko hai ni kwa neema tuu na pia tupo kwa ajili ya kumwabudu Mungu wetu na ili tuweze kutimiza wajibu huu katika viwango Mungu anavyohitaji anatukumbusha tutubu Naye ni mwaminifu anatusamehe na kutufutia uovu wetu na tunaendelea na safari ya kumtumikia kwa faida.
Na katika kuchukua hatua ya kujitathmini wapi tunamhuzunisha Mungu ili tutengeneze, Roho Mtakatifu ni mwaminifu atatukumbusha kila eneo lililodhaifu ili tuendapo mbele za Mungu kwa toba tutengenezwe sawasawa.
Baada ya toba itakayoongozwa na Roho Mtakatifu unatakiwa uamini kuwa Mungu amekusamehe na wewe mwenyewe ujisamehe. Kuna namna nafsi huwa inatuhukumu kwa kutukumbusha dhambi ambazo tulizifanya lakini pia tulishazitubu. Unatakiwa kuinyamazisha kuiambia hakika niko huru!!! Ulishasamehewa!!!! Kwa ujasiri kabisa.
Ninewiwa kuzungumzia hili kwa sababu watu wengi baada ya kuanguka na kutubu huwa wanapata bumbuazi La rohoni kwa nafsi kuwashtaki kila mara ambayo inawanyima ujasiri wa kwenda mbele za Mungu. Na ikiendelea kwa Muda mrefu utajikuta unaacha kumkaribia Mungu ambayo ni hatari sana kwa afya yako ya kiroho na ya kimwili.
Tujihimize kutubu na kutenda sawa na neno la Mungu linavyotuagiza.
Mbarikiwe sana kwa Utukufu wa Mungu.
Na: Batilda Raphael
Kujiunga na darasa letu la watsapp tuandikie +255758358236