JE KUFANIKIWA KWAKO KUNATEGEMEA NINI?
Mtu yeyote aliyeokoka anao uwezo wa kuishi na kuwa na uhakika
ama atakuja kufanikiwa katika maisha ama hatofanikiwa.Nina maana kwamba mtu
yeyote aliyeokoka anaweza kujua wapi anaelekea kabla ya kupafikia. Kwa sababu ifuatayo;
·
Mtu
aliyeokoka ana uwezo wa kumuuliza Mungu kwa habari ya mambo yatakayokuja.
“BWANA ,Mtakatifu wa Israeli na Muumba wake asema
hivi, Niulize habari za mambo yatakayokuja;mambo ya wana wangu na habari ya kazi
ya mikono yangu,haya!Niagizeni.” Isa 45:11
Kama Mungu anatupa mwaliko wa kwenda na kumuuliza habari za
mambo yatakayokuja sasa ni kwa nini mtu aliyeokoka ashindwe kuyajua maisha yake
yajayo?.Tatizo la watu wengi waliookoka ni wazuri katika kuombea mapepo ama
kuziombea huduma mbalimbali ila sio kuyaombea maisha yao.
Na ili swala la kumuuliza Mungu habari zitakazokuja ni la mtu
binafsi sio la kikundi.
·
Mungu mwenyewe anaweza kujifunua
kwako na kukupasha habari zako zijazo.
Sote tunakumbuka haikumuhitaji Yusufu kufunga na kuomba ili
Mungu amwambie habari za maisha yake yajayo isipokuwa Mungu mwenyewe alijifunua
kwa njia ya ndoto. Mwanzo 37:3-6
Kuna watu leo tunao ndani ya kanisa ambao Mungu alikwisha
sema nao mahali watakuwepo kwa njia yoyote ile aliyosema nao lakini bado
wanaishi kwa kubahatisha.Tatizo la watu wengi nimegundua sio kusemeshwa
isipokuwa kuelewa kile walichosemeshwa.
Watu wengine wengi
wamekwama katika maisha kwa kufikiri kufanikiwa kwao katika maisha kunamtegemea
mtu.Biblia inatupa kuona ya kwamba mtu hafanikiwi kwa sababu kuna mtu aliomtoa
isipokuwa tunachokiona ni kwamba mtu anafanikiwa kwa kuletewa msaada na Mungu.
Kufanikiwa kwako hakutegemei wala hakuzuiwi na sababu yoyote
ile uliyo nayo. Kwa mifano;
1. Sababu za kimadhingira
Kuna kundi kubwa sana la walokole wamezidi kubaki katika hali
zao kutokana na kuamini kwamba maeneo waliyopo hawawezi kufanikiwa.
Unapaswa kujua kwamba hakimpi Mungu shida wewe kuzaliwa
familia uliyozaliwa.Kuna watu wakiangalia historia za maisha yao kiuchumi
hawafikiri kabisa ya kwamba yuko Mungu ambaye anaweza kupita katikati na
kubadilisha hali yao ya maisha.Umewai kufikiri kama Daudi kwa madhingira ya
kifamilia aliyokuwa akiishi angeweza kutoka kimaisha hadi kuwa mfalme? 1Sam
16-17
Hakimpi Mungu shida ya kwamba umesoma vidato vingapi ndipo
hakufanikishe katika maisha.Watu wengine wengi wamekwama tu eti kwa sababu
wanajiona wajasoma kabisa.Mimi sijui ni nani aliyekwambia kama hujasoma huwezi
kufanikiwa.Ingekuwa kusoma ni kufanikiwa basi kila aliyesoma ungemuona akiishi
maisha mazuri.Sasa kwa sababu watu wengine hawajasoma basi wamejitengenezea
mipaka sana katika maisha yao.,kwa mfano
utakuta mtu ana karama ya kuhubiri lakini hajawai hata siku moja kwenda
kuwahubiri wasomi akifikiri sio saizi yake.Ivi umewai kuona ni wapi katika
biblia Yesu anaenda shule?lakini bado huyu huyu Yesu tunaona anawashinda
wanasheria wa kiyahudi.Sasa sina maana ya kwamba kusoma ni kubaya hapana.
Ile kwamba kabla ya kuokoka umekuwa mdhambi sana si sababu ya
Mungu kutokufanikisha leo ulipoamua kumuishi naye.Watu wengi wamewai kusikia
ndani yao hali ya kutaka kumtumikia Mungu na wanaposikia hivyo mara moja
wanaona mafanikio mbele yao lakini kiko kitu kinawahukumu ya kwamba
hawawezi.Ingekuwa ni hivyo basi Paulo asingefika popote kitumishi kwa sababu historia
yake ya kimadhingira ilikuwa ni mbaya sana
Mdo 6-.Akina Rahabu basi
wasingefika popote kama ni vivyo maana Rahabu historia yake ya kimaisha sote
tunaijua Yoshua 2.Unajua nimesema
hii kitu kwa sababu walokole wengi ambao neema ya Mungu ilifunuliwa kwao kabla
na wakaishi maisha ya kiroho mapema wanawahukumu wenzao eti.Kuna wadada
wanafikiri kwa sababu hawakuwai kufanya uzinzi basi wamestahili sana kuliko
wenzao.Sasa unielewe vizuri sina maana uzinzi ni mzuri.
2. Sababu za kiumri
Watu wengine wamejitazama idadi ya miaka waliyo nayo
wakafikiri ni kigezo cha wao kutokufanikiwa.Wengine umri kwa sababu ni mdogo
wamefikili hawawezi kufanya vitu wakafanikiwa.Na sijui nani kawambia hiyo
kitu.Na hata kanisa nalo limewakwamisha watu wengi sana wasipige hatua kwa sababu
ya umri walio nao.Utakuta watoto wadogo katika kanisa wanawekwa nyuma nyuma kwa
sababu wao ni wadogo.
Mifano;
·
Mfalme
Uzia,1nyak 26:3
·
Mfalme
Manase,1nyak 33:1
·
Mfalme
Yosia,1nyak 34:1
Sasa kama Mungu aliwatumia akina Yosia mabwana wadogo kiasi
hicho kwa nini wewe angoje uwe mkubwa ndipo akutumie?
Watu wengi hawafahamu hii kitu,Mungu akitaka kukutumia
hakuhakikishi idadi ya umri wako isipokuwa kuna vitu ni vya muhimu ambavyo huwa
anavihakikisha.Na akivikuta viko sawasawa ndipo anakuinua na kukutumia pasipo
kuangalia kigezo chochote ulicho nacho.
Mfano wa Yeremia.
“Tena neno la Bwana likanijia kusema,Yeremia waona
nini?nikasema naona ufito wa mlozi.Ndipo Bwana akaniambia umeona vema kwa maana
naliangalia neno langu ili nilitimize.Neno la Bwana……………….” Yer 1:11-12
Kabla ya kukuinua katika huduma na kukufanikisha haya ni
baadhi ya mambo Mungu anayoyahakikisha;
i.
Fikra
yako
ii.
Macho
yako
iii.
Kusikia
kwako
Macho ya Yeremia
Hapo alichokuwa anakifanya Mungu ni kuyahakikisha macho ya
Yeremia kama yanaona sawa sawa.
Fikra zako.
Kinachoweza kukuweka katika uongozi mkubwa katika ngazi ya
siasa si umri wako ni fikra zako juu ya mambo.Watalaamu wanasema hivi “Leadership is not a position but an
altitude.”maana yake ni kwamba unaweza ukawa na nafasi ya kuwa kiongozi
lakini usiwe na fikra za uongozi.
Umri wako kuwa mkubwa pia sio sababu ya Mungu
kutokukufanikisha.Watu wengi sana ambao umri umekwisha sogea wanakuaga na fikra
potofu za kutokufanikiwa.
“Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi asema Bwana,ni
mawazo ya amani wala si ya mabaya,kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.”
Yer 29:11
Watu wengi wenye umri mkubwa wanaamini ya kwamba kama umri
umepita wakashindwa kujikusanyia mali basi hiyo kitu hawawezi kuifanya katika
umri wao.Hata mimi naungana nao kusema hivyo ya kwamba kama haukuwa tajiri
wakati wa ujana wako huwezi kuwa tajiri siku zako za uzee kufuatana na mtazamo
wa kisiasa.
Lakini mtazamo wa kibiblia uko tofauti kidogo,maana biblia
inasema izo siku za mwisho kufanikiwa UTAPEWA na sio utatafuta.
Na kuna baadhi ya wazee wanajidanganya ya kwamba umri wa
kuishi ni miaka sabini ila ukiwa na nguvu ni themanini.Zab 90:10……Mwa 6:3
SASA KUFANIKIWA KWAKO UWE NA UHAKIKA KUNATEGEMEA UNAVYOISHI
NDANI YA KUSUDI AMBALO MUNGU AMEKUITIA KULIFANYA HAPA DUNIANI.
Ni vigumu sana kufuatana na ushauri wa kibiblia ukafanikiwa
nje ya kusudi lako Mungu alilokuitia.Kwa hivyo ni lazima au ni muhimu kujua
kitu ambacho Mungu amekiweka ndani yako na ukajua thamani ya hiko kitu.
Kwa mfano;
Kama nyumbani kwako chini ya ardhi kuna madini halafu
haukujua siku utakopoamua kupauza hapo utapauza kwa bei rahisi sana.Kama
hautojua wewe ni nani hautojua thamani yako katika ulimwengu huu.
Ukiwa unafanya mambo ndani ya kusudi ambalo Mungu amekuitia
kitu ambacho kinatokea ni kwamba mtu wako wa ndani anafanikiwa sana hadi
kusababisha mtu wa nje kufanikiwa pia.
“Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yako na afya yako kama
vile roho yako ifanikiwavyo.” 3Yoh 1:2
Mtu yeyote aliyefanikiwa hapa duniani alianzia rohoni kabla
ya mwilini.Ndiyo maana biblia inatuambia cha kwanza kutafuta ni ufalme then
vingine tutazidishiwa.
“Bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake na hayo
yote mtazidishiwa.” Math 6:33
Hata wachawi wanaijua hii kanuni ya mafanikio ya kwamba
mwilini kunafata baada ya rohoni kufanikiwa.
Kusudi kubwa ambalo Mungu amemwitia mwanadamu ni utumishi katika shamba lake.
1Kor 12:12-21+efe 4:15-16
Siku zote tunaishi ili tuujenge mwili wa Kristo na kwa
kufanya hivyo tutakuwa tumetumika ndani ya kusudi la Mungu.Sasa katika kuujenga
mwili wa Kristo wengine ni
·
wajenzi
wa nje na
·
wengine
ni wa ndani.
Ukijua wewe unakitu gani kiatamie katika maombi hadi kiwe
dhairi mbele ya mioyo ya watu. Kwa mfano Yusufu alijua mapema sana tangu akiwa
na umri wa miaka kumi na saba yeye ni nani katika taifa. Mwanzo 37:5-8
Lakini siku ilipofika hata wakuu wa nchi walijua ya kwamba
hakuna mtu kama Yusufu kwa hivyo lazima wamtafute yeye.
Soma Mwa 40:1-15
Mambo tunayojifunza
kutokea hapo.
a.
Usimuhudumie
mtu kwa nguvu yote ya wito wako kwa sababu ya jinsi alivyo.
Tatizo la watu wengi wamegeuza utumishi wao kama source ya
kupata pesa.Kwa mfano kilichomcost Yusufu alizani kwa kuwa amemuhudumia basi
ataomtoa kimaisha yule mwokaji wa Mfalme ndio sababu alimwambia akitoka
asimsahau.
b.
Usichague
eneo la kumtumikia Mungu, ile tu Mungu kakuhakikishia nenda.
Yusufu angetazama kwa jinsi ya nje asingejisumbua kumtafsiria
ndoto yule ndugu gerezani maana asingempa chochote even sadaka.Sasa kuna watu
wengi wameshindwa kufanikiwa japo wako ndani ya kusudi la Mungu kwa sababu ya
kuchagua chagua maeneo makubwa na yenye hadhi kwao.Utakutana na mtu kabisa
ndani yake anaona kiu ya kufanya biashara fulani lakini anajiona kama
atajishusha hadhi yake vile.
c.
Sababu
za kimadhingira si kigezo cha wewe kutokufanikiwa.
Sio rahisi kukubaliana na hali aliyokuwa nayo Yusufu, maana
ametoka gerezani hadi kuwa mkuu wanchi. Si rahisi kufikiri kama angeweza
akatokea mtu na kumuokoa toka kule gerezani na kumpandisha.
MAMBO SABA
YANAYOWEZA KUCHOCHEA MAFANIKIO YAKO.
Kitabu cha Yoshua
1:6-9 kinatuelekeza mambo hayo saba hapa chini;
i.
Kuwa
hodari/be strong
ii.
Kuwa
na moyo wa ushujaa/have courage
Having courage is about facing our fears and moving on in
faith.
iii.
Msikilize
baba yako wa kiroho
iv.
Lifanye
neno la Mungu kama lako.
Ukiligeuza neno la Mungu kama ni lako itakupa urahisi wewe
kulitafakari jinsi linavyohusika na maisha yako ya kila siku.Mungu alipomwambia
Yoshua kitabu cha torati kisiondoke maana yake alitaka kiwe chake.
“Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako,bali
yatafakari maneno yake usiku na mchana……..”
Tatizo linalowakumba wakristo wengi badala ya kutafari neno
la Mungu wanatafakari ukubwa wa shida walizonazo.
v.
Fata
kile Mungu anakwambia kufanya.
vi.
Anza
kufanya jambo unalolisikia ndani yako./weka katika matendo ndoto yako.
Kama utakumbuka wakati ule wana wa Israeli wako katika bahari
ya shamu maji hayakuwanyika hadi wameweka miguu yao ndani ya maji.Ni hatari
sana ukaa na ndoto kichwani au moyoni isiyowekwa katika matendo.Wengi
wameshindwa kuweka ndoto zao kwenye matendo kutokana na madhingira waliyo nayo.
vii.
Usiogope