UKO TAYARI KUTUMIWA BILA KUMJUA MUNGU ANAYEKUTUMIA?
Isaya 45:
4 Kwa ajili ya Yakobo, mtumishi wangu, na Israeli, mteule wangu, nimekuita kwa jina lako; nimekupa jina la sifa; ijapokuwa hukunijua. 5 Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu; nitakufunga mshipi ijapokuwa hukunijua;
Mungu.anaposema, Neno na kulirudia mara zaidi ya moja inafanya mtu usikilize kwa Makini. Amemitwa Koreshi na Kumsimamisha kama Mtumishi wake na akatangaza kumtumia kwa namna ya ajabu na kumpa Jina, ila cha ajabu anamwambia, Mie pamoja na Kufanya hayo yote kwako lakini HUNIJUI.
KUTUMIWA na Mungu sio kigezo cha Kupima Uhusiano wako na Mungu. Ili pawe na Uhusiano lazima Umjue Mungu. Lakini kwa maneno haya ya Mungu kwa Koreshi ni wazi kuwa kulikuwa hakuna UHUSIANO kati ya Mungu na Koreshi.
Sasa inaachilia Swali, Mungu unayemtumikia Unamjua..!?? Musa alipoitwa Mungu alimwambia Umepata Neema nami Nimekujua jina lako, ila Musa hakutosheka aling'ang'ania Kumwambia Mungu,,, Wewe ni Nani,..!!!?
Musa hakubweteka na Kuitwa na kujulikana na Mungu,yeye alitaka KUMJUA MUNGU. Usije ukafikiri kwasababu mtu fulani anatumika na Mungu kwa kiwango kikubwa, ukahitimisha kuwa anamjua Mungu.
Musa hakubweteka na Kuitwa na kujulikana na Mungu,yeye alitaka KUMJUA MUNGU. Usije ukafikiri kwasababu mtu fulani anatumika na Mungu kwa kiwango kikubwa, ukahitimisha kuwa anamjua Mungu.
Usiridhike tu, Mungu kukujua, tafuta Kumjua yeye...!!!
Yoh 10
Yoh 10
14 Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi; 15 kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. 16 Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.
Yesu aliamua kuliweka wazi swala la uhusiano kati ya mtu na Mungu kwa kusema kwamba Yeye anawajua na wao wanamjua. Kutokumju Yesu ni ishara tosha kwamba wewe sio wake. Kama una uhakika wewe ni wake hakikisha una uhakika kwamba unamjua.
Kama vile Mungu alisema kuwa Koreshi HAMJUI japo Yeye anamjua, ndicho kitu Yesu anasema wako walio nje ya zizi na anawajua ila wao hawamjui"Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili" . Kiu ya Mungu iliyo msukuma atoe uhai wa Yesu ni ili kila mtu amjue na awe na uhusiano nae. Unaweza kumjua Yesu kupitia neno lake maana Yeye ni Neno.
Yoh 1
1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Neno anayezungumzwa hapa ni Yesu, sasa ukitaka kumjua Yesu soma Neno lake