Header Ads

YESU NI MZABIBU-SEHEMU YA PILI


JAMBO LA TATU
Yesu ni mzabibu nasi tu matawi
Isaya 5
7 Kwa maana shamba la mizabibu la Bwana wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza; akatumaini kuona hukumu ya haki, na kumbe! Aliona dhuluma; alitumaini kuona haki, na kumbe! Alisikia kilio.
Nataka uone hili neno “Yuda ni mche wake” kisha linganisha na neno “mimi ni mzabibu”. Kumbuka Isaya anasema “Nyumba ya Israel” ndio shamba la Bwana. Maana yake kutokea kwenye shamba linaitwa nyumba ya Israel amempanda Yuda kama mche/mzabibu/mzabibu ulio mzuri.

Sasa rejea mfano wa shamba la mizabibu na mzabibu mwitu uliozaliwa. Mungu alipoingia gharama ya kumtafuta Daudi alitegemea nyumba ya Yuda (mche) ungetoa zabibu njema matokeo yake ukatoa zabibu mwitu. Mungu alitumai kuona hukumu ya haki kumbe aliona dhuluma (zabibu mwitu), alitumaini kuona haki na kumbe kilio. Kwa ivyo moja ya matunda unapaswa kuzaa ukiwa ndani ya Yesu ni haki. Sasa ni kazi ndogo jitathimini inapofika kusimamia haki unakua upande gani?

Yer 23
5 Tazama siku zinakuja, asema Bwana, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi.
Isaya 11
1 Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda.

Sababu ya Yesu kujiita mzabibu ilitokana na kwamba yeye ni chipukizi. Chipukizi sio mti halisi isipokua ni mti ulio chomoka kwenye mti uliokuwepo ukalala bila kuota. Kwenye nyumba ya Yuda kuna kitu Mungu alikua akikigharamikia kikampa matokeo asiyo tarajia. Kwa ivyo ilibidi amuandae mtu toka kwenye nyumba ya Yuda. Sasa kama yeye ni chipukizi ndio sababu anajiita mzabibu huku akijua kuna mwenye shamba la mizabibu na ana matarajio na ilo shamba kuzaa kitu.

Mzabibu na Matawi
Ayu 14
8 Ijapokuwa mizizi yake huchakaa mchangani, Na shina lake kufa katika udongo;

9 Lakini kwa harufu ya maji utachipuka, Na kutoa matawi kama mche
Mzabibu ulitegemewa kutoa matawi (mimi na wewe) yanayosemwa hapa ndiyo yale kwenye Yohana 15

JAMBO LA NNE
Idadi ya vilivyo zaliwa

Yoh 15
2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.

“Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa” kama Yesu angekuwa ni yeye mwenye kuondoa ilo tawi lisilo zaa angesema “naliondoa”. Kusema huliondoa maana yake hiyo sio kazi yake ni kazi ya mwenye shamba. Maana yake ni kwamba mkulima yuko kifaida kuliko tunavyoweza kuzani. Yeye hakimsumbui kuwa ndani ya Yesu kinachompa shida ni kuwa ndani ya Yesu bila kuwa na faida. Kwa ivyo hana huruma kusema akuache kwa kuwa uko ndani ya Yesu, atakuondoa tu.
Nataka uelewe kwamba kuna watu wako ndani ya kanisa na niwazuri sana ndani ya Yesu lakini hawana faida yoyote ile. Mbingu utaiona ila utatembea chini ya kiwango ukiwa hapa duniani.


Mfano wa Kabaila
Luka 19
2 Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi.
13 Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja.
15 Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake.
16 Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi.
17 Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.
20 Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso.
21 Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda.
22 Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;
26 Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang'anywa hata alicho nacho.

Huu mfano wa kabaila Yesu anataka tujue umuhimu wa kumzalia matunda/ kumtengenezea faida. Huyu mjakazi mpumbavu huenda akawa anawakilisha wakristo wengi sana ambao ni mahodari wa kushiriki ratiba zote za kanisa lakini sio wazalishaji wa chochote katika kumtengenezea Yesu faida. Jiulize una watu gani unajivunia kuwa ulimzalia Yesu tangu akupe neema uokoke?

Itaendelea.....
Theme images by centauria. Powered by Blogger.