YESU NI MZABIBU-SEHEMU YA KWANZA
Yoh 15
1 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.
5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
Mambo
ya kuelewa
- Yesu aliposema yeye ni mzabibu na kuwaita wanafunzi wake matawi kiu yake ya kwanza ilikua ni wao kuwa na uwezo wa kuzaa sana. Kama ingelikua anawapima maana yake kipimo chao cha kwanza kingekua ni idadi ya vilivyo zaliwa sio kitu kingine.
- Yesu kajitofautisha na aina zingine za mizabibu kwa kujiita “mzabibu wa kweli”. Hadi amejiita ni mzabibu wa kweli maana yake ni kwamba kuna mizabibu isiyo ya kweli.
- Yesu amejitambulisha kama mzabibu na kutambulisha anachokitarajia kwa wanafunzi wake kwamba ni kuzaa sana bila kueleza kazi za mkulima na matarajio ya mkulima.
- Yesu kutomzungumzia Mungu kama mkulima na matarajio yake kunafanya kutoona kama mkulima ni wa muhimu
- Walio itwa ni matawi ni ishara kwamba hawajitosherezi bila mzabibu. Kufanikiwa kwao kunategemea mzabibu.
JAMBO
LA KWANZA
Mzabibu
wa kweli
Unaposoma biblia neno
“mzabibu” kwa sehemu kubwa limekua likimaanisha watu wake yaani Israel. Zab
80:8-9
Isaya 5
1 Na nimwimbie
mpenzi wangu wimbo wa mpenzi wangu katika habari za shamba lake la mizabibu. Mpenzi wangu alikuwa na shamba la
mizabibu, Kilimani penye kuzaa sana;
2 Akafanya handaki kulizunguka pande zote,
Akatoa mawe yake, Akapanda ndani yake mzabibu
ulio mzuri, Akajenga mnara katikati yake, Akachimba shinikizo ndani yake;
Akatumaini ya kuwa utazaa zabibu, Nao ukazaa
zabibu-mwitu.
Mmiliki wa shamba
anaoneka kuwa na shamba la mizabibu (wingi) lakini anaonekana kupanda mzabibu
(mmoja) ulio mzuri. Hii ina maana kwamba katika shamba lake la mizabibu kuna
mzabibu alio upanda ambao uko tofauti na mizabibu mingine. Yesu anaposeama yeye
ni mzabibu wa kweli maana yake ni kwamba anajitofautisha na mizabibu mingine
isiyo ya kweli (isiyo mizuri). Kama zabibu mwitu imezaliwa ikiota nayo itaitwa
mzabibu, usipoambiwa huu ni mzabibu wa kweli unaweza kuutumia kumbe ni mzabibu
mwitu.
Kwa ivyo jambo
tunaloliona hapa ni kwanza kabla ya kujiweka kwenye mzabibu lazima kujua aina
ya mzabibu. Jesus is
the true vine. We must be rooted in Him (not in Israel) if we
will bear fruit for God. In the New Covenant community, our first
identification is in Jesus Christ Himself, not in Israel or even in
the church as such. Math 21:33-40
Unawezaje
kufahamu mzabibu wa kweli
Yoh 8
31
Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno
langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;
32 tena mtaifahamu
kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru
Ukiona mtu anatumia
neno kukufundisha na mwisho wa siku hupati uhuru, ni dalili tosha umeegemea
kwenye mzabibu usio wa kweli.
JAMBO
LA PILI
Yesu kutokumzungumzia
mkulima kunafanya tusijue mambo yafuatayo
- Gharama alizotumia mkulima kulima
- Matarajio ya mkulima kwa kile alicho kilima
- Kinachotokea mkulima asipokipata alichokitarajia
Gharama
za Mkulima
Isaya 5
1 Na nimwimbie
mpenzi wangu wimbo wa mpenzi wangu katika habari za shamba lake la mizabibu. Mpenzi wangu alikuwa na shamba la
mizabibu, Kilimani penye kuzaa sana;
2 Akafanya handaki kulizunguka pande zote,
Akatoa mawe yake, Akapanda ndani yake mzabibu
ulio mzuri, Akajenga mnara katikati
yake, Akachimba shinikizo ndani yake; Akatumaini
ya kuwa utazaa zabibu, Nao ukazaa zabibu-mwitu.
4 Je! Ni kazi gani
iliyoweza kutendeka ndani ya shamba langu la mizabibu nisiyoitenda? Basi,
nilipotumaini ya kuwa litazaa zabibu, mbona lilizaa zabibu-mwitu?
- · Mkulima aliloligharamikia ni kutafuta eneo zuri la uzalishaji lenye uwezo wa kuzaa sana.
- · Mkulima lihakikisha anapanda mzabibu mzuri
- · Mkulima aliweka ulinzi wa kutosha
Matarajio
ya mkulima
Kilichomfanya mkulima
awe na matarajio mazuri ni kwa sababu aliweka kila kinachohitajika ili shamba
lake lizae vizuri. Mkulima katika hali ya kawaida anaweza asiwe na matarajio
makubwa juu ya shamba lake endapo atakua hajalihudumia katika kila kitu
kinachohitajika. Kilichotokea ni mzabibu kuzaa zabibu mwitu, kitu ambacho
kilikua kinyume na matarajio ya mkulima. Embu jaribu kuweka haya maneno kwenye
Isaya 5:4
4 Je! Ni kazi gani
iliyoweza kutendeka ndani ya shamba langu la mizabibu nisiyoitenda? (nimekupa
uhai, nimekulinda na ajali, nimekupa kazi, nimekupa chakula n.k). Basi,
nilipotumaini ya kuwa utanizalia matunda umekua msikilizaji tu kila siku
kanisani wala hujishughulishi kuhakikisha unahudumia wengine, mbona umezaa dini
badala ya wakristo?
Kinachotokea
mkulima asipopata alichokitarajia
Isaya 5
5 Haya basi,
sasa nitawaambieni nitakalolitenda shamba langu la mizabibu; nitaondoa kitalu
chake, nalo litaliwa; nitabomoa ukuta wake, nalo litakanyagwa;
6 nami nitaliharibu;
wala halitapogolewa wala kulimwa, bali litamea mbigili na miiba; nami
nitayaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.
Hii ilikua ni matokeo
sio ya kutokuzaa, hapana ila yalikua ni matokeo ya kuzaa
kisichotarajiwa. Ukisoma hii Isaya utaona tatizo halikua kutokuzaa isipokua ni
kuzaa kitu kisicho sahihi (mzabibu mwitu). Hayo mambo yote juu kutokana na
kutokuzaa kitu sahihi yakaondolewa
Itaendelea.....