UMILIKI KATIKA UFALME
Shalom
Leo tujifunze kidogo kuhusu
umiliki katika ufalme. Hii inalenga namna ambavyo Mungu anamiliki vitu na
shetani anavyomiliki. Katika kuelewa tuangalie angalu kwa ufupi, namna Yesu
alivyoulizwa na mafarisayo kuhusiana na dinari, baada ya kumpamba kwa maneno
mazuri.
Wakasema;
“Tuambie basi, Wewe unaonaje? Ni halali
kulipa kodi kwa Kaisari au la?’’ Lakini Yesu akijua makusudi yao mabaya
akawaambia, ” Enyi wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega ? Nionyesheni hiyo
sarafu inayotumika kwa kulipia kodi. ” Wakamletea dinari. Naye akawauliza,
”Sura hii na maandishi haya ni vya nani ?” Wakamjibu, ‘‘Ni vya Kaisari.’’ Basi
Yesu akawaambia, ‘‘Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho
cha Mungu.’’ (Mathayo 22:17-20)
Sentensi hii inajengwa kwamba yeye aliye
na chapa katika kitu ndiye mmiliki na anakistahiri hicho kitu. Inawezekana
mafalisayo hawakumwelewa kwa sababu ilikuwa sentensi ya kifalme. Mtu anapotaka
kumiliki kitu chake kihalali, anaweka mhuri au chapa yake na mtu mwingine
hawezi kuchukua.
Yesu anawaambia kama dinari hii ina chapa
ya kaisari, Kaisari anaistahiri kwa sababu ni milki na muda wowote anaweza
kuihitaji (Claim), lakini ingekuwa na chapa ya Mungu, haisari angepoteza
uhalali na kwa sababu hiyo angepewa Mungu.
Ona, Shetani anapotaka kutawala na
kukimiliki kitu anakiwekea chapa yake, kuonesha kwamba anaweza kuhitaji na
kukitumia muda wowote. Na Mungu hivyo hivyo. Kabla ya kuokoka kwa mtu, Shetani
anakuwa na chapa yake, kwa hiyo atamtumia muda wowote anaomhitaji (He can claim
that person any time). Lakini anapookoka, damu ya Yesu inatangua ile chapa
(umilki) ya shetani na kuweka chapa yake.
“Ninyi pia mliingia ndani ya Kristo
mliposikia Neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Mkiisha kuamini, ndani yake
mlitiwa MHURI, kwa yule Roho Mtakatifu wa ahadi mliyeahidiwa, yeye ndiye amana
ya urithi wetu hadi ukombozi wa milki yake kuwa sifa ya utukufu Wake”. Efeso
1:13-14
Kama shetani ameweka mhuri katika sehemu
fulani ya maisha yako, na unashindwa kutoka hapo, utangue huo mhuri kwa damu ya
Yesu na weke mhuri wa Roho mtakatifu. Alafu mwambie, Mungu ndiye animilikie
wala sio wewe. (God own me and I belong to Him).