GBS IMEBADILISHA MAISHA YA WAKRISTO
“Graedy Bible Study” (GBS) ni darasa la kusoma biblia kila siku kwa njia ya mtandao lililo chini ya Graedy International (GI). Kwa kiasi kikubwa darasa hili limekua likifanyika kwa njia ya “watsapp” na kuwafikia wakristo wengi tangu lianzishwe. Hadi sasa GBS imefikia zaidi ya wakisto 150 toka sehemu mbalimbali ndani na nje ya dar es salam. Msisitizo wa GBS unajengwa na Neno kutoka Kol 3:16 “Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenukatika hekima yote…….” Ukiwa na lengo la kuwajengea wakristo tabia binafsi ya kusoma, kulitafakari na kulitumia Neno la Mungu kila siku ili kubadilisha maisha yao bila kusubiri wakati wa ibada pekee. Hii ni kumsaidia mkristo angalau kusoma na kuimaliza biblia. GBS inaongozwa na kauli mbiu “Jifunze kwa kuandika” yenye lengo la kujenga uwezo na tabia binafsi ya kuandika kile Roho Mtakatifu anamsemesha mtu kupitia Neno.
Mr Elton Simoni Matandala
ni kijana aliyeokoka na kumpa Yesu maisha yake kutoka Kanisa la Kiinjili la
Kiluteli Tanzania Usharika wa Kiluvya, Kiluvya gogoni. Mr Elton alijiunga na
GBS mwezi wa pili mwaka 2016 baada ya kusimuliwa habari za GBS na Mwalimu wake
wa Neno la Mungu aliyekuwa mshiriki ndani ya darasa ilo. “GBS imenibadilisha sana, kabla ya kujiunga na GBS nilikua nasoma biblia
vimistari vichache kisha nalala, wakati mwingine sisomi kabisa na hata kanisani
walikua wakisema tuwe na tabia ya kusoma biblia halikua jambo linalo niumiza
sana. Nilipojiunga na GBS mambo yalibadilika kabisa juu ya usomaji wangu wa
biblia na kutafakari. Nilianza kusoma kitabu kwa kitabu na kutafakari mstari
kwa mstari kwa lengo la mimi kupata kitu kisha kuwashirikisha na wengine.
Vitabu kama “Hesabu”, “Mambo ya Nyakati, “Mambo ya Walawi” sio vitabu nilikua
naweza nikavisoma ila sasa nimevisoma. Kwa kweli ninaona badiliko ndani yangu.
GBS imenisaidia sasa ninao uwezo na ujasiri wa kuandaa somo sawa na maelekezo
ya Roho Mtakatifu na kuhubiri.”
Mr Elton anakumbuka jambo
moja kubwa kutokea kwenye maisha yake mnamo tarehe 3/07/2016 alipata kibali cha
kuhubiri kwenye ibada ya vijana ndani ya usharika anaosali. “Nimekua nikuhubiri nikiwa na Ushirika wa Kikristo wa Wanafunzi (UKWATA)
wakati niko sekondari, ila hii naona ni ya kiwango cha juu ukilinganisha na
nilikotoka” Ilo jambo
anaeleza kuwa ni matokeo ya ujasiri uliojijenga kwake kupitia darasa la GBS na
limeweka alama kubwa ndani ya moyo wake katika kumbukumbu za maisha yake.
Ameanza kujua thamani yake aliyo nayo ndani ya Kristo Yesu na nini kinampasa
kufanya kwa ajili yake na kwa ajili ya kuwasaidia wengine. Hadi sasa Mr Elton
Mungu amemsaidia na kumtumia kuhudumia watu wa rika mbalimbali.
Mr Elton alipoulizwa nini hasahau alichojifunza kwenye biblia akiwa na GBS NI juu ya alichokisoma kwenye kitabu cha Samweli kuhusu Daudi. Daudi pamoja na
kutafutwa muda mrefu na Sauli mfalme kwa lengo la kutaka kumuua. Siku moja
Sauli alipatwa na usingizi na Daudi alikua kwenye nafsi ya kumuua adui yake
lakini hakufanya ivyo kwa kuogopa kumfanyia ubaya masihi wa Bwana. “Adui yako mwenye kushughulika naye ni Mungu mwenyewe. Adui
anayepambana na kusudi la Mungu lililo ndani ya maisha yako sio wa kumlipizia
atashughulikiwa na Bwana mwenyewe. hili tukio sitokuja nisahau kwenye maisha yangu, limekua funzo kubwa dhidi ya maadui wangu”.
Ukitaka kujiunga na darasa letu la watsap gonga jiunge nasi kupata maelekezo.
Ukitaka kujiunga na darasa letu la watsap gonga jiunge nasi kupata maelekezo.