Header Ads

SHUKRANI

Mhubiri 3:4 “Kuna wakati wa kulia na wakati wa kucheka”
Kunaweza kuwa na tafasili nyingi kadri Roho wa Mungu anavyoweza kuweka kiu ndani ya moyo wa mtumishi wake. Leo tutazame hili andiko juu ya hizi nyakati mbili “kulia” na “kucheka” kwa maana ya kukosa kile ulichokusudia kukipata. Mtu anaweza kweli kulia kwa kukosa kile alichokusudia kukipata ila aliye ndani ya Kristo hatutarajii kukuta ana wakati wa kulia juu ya kile alichokikusudia na hakakosa. Wakati wa kulia upo kwa mtu aliye nje ya Kristo Fil 4:4, 1Thes 5:16 “Furahini siku zote”

Wakati wa kucheka
Huu wakati wa kucheka twende na maana kwamba wakati ambao mambo yako yanakwendea vizuri. Sasa agano jipya linachokitaka ni kwamba yameenda vizuri au vibaya ile tu kwamba uko ndani ya Kristo furahi.

Sasa angalia hapa: -
1Thes 5:18 “Shukuruni kwa kila jambo maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu”. Ukisoma kwa tafasili ya kiswahili ninachotaka ukione hutokiona. Let read it in Holy Bible (ESV) “give thanks in all circumstances for this is the will of God in Christ Jesus for you”

“in all circumstances”
Nilitaka uone ilo neno. Kwa tafasiri isiyo rasmi ya kiswahili ni “ukiwa ndani ya hali zote”.
Maana yake ni kwamba incase uko ndani ya majanga tayari au uko ndani ya hasara yani biashara haijaenda sawa hapo ndipo pa kushukuru Mungu maana kama ulikua ndani ya Kristo hayo ni mapenzi yake kwako. Sasa huwezi kufanya iyo shukrani kama kuna wakati unalia. Hii ili kuiweza kuifanya lazima ufurahi siku zote. Kulia wakati ulilolikusudia hujalipata ni kujiandaa tu kulalamika na sio kushukuru. Ninaelewa ukowakati unaweza kulia kwa lengo la kuondoa uchungu ulio nao bila kulalamika.

Jaribu kufikiri una mwanamke kisha gafla baada ya kufanya hatua zote ili umuoe linatokea jambo la kuwatenganisha. Kama uko ndani ya Kristo yakupasa tu ufurahi kisha umshukuru Mungu.  Nasema ivi kwa sababu huenda kuachana na huyo mwanamke ni Mungu kakuepusha kufuatana na Mhubir 7:26

“Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti, yaani mwanamke ambaye moyo wake ni mitego na tanzi, na mikono yake kama vifungo; yeye ampendezaye Mungu atamponyoka bali mwenye dhambi atanaswa nay eye”.  Maana ikiwa ataacha uoe hapo ndio kusema umejichomoa jumla ndani ya mapenzi yake.

Lengo:-

Nimesema haya yote ili tunapo mshukuru Mungu kwa yote tuliyokuwa nayo ndani ya mwaka huu tumshukuru kwa uhalisia kabisa. Huenda kuna vitu ulikusudia vitokee mwaka huu vijatokea mshukuru Mungu. Huenda iyo kazi uliyo ndani yake sasa si ile uliikusudia mshukuru Mungu hata ukiwa ndani ya ilo usilolipenda ni mapenzi yake kwako uliye ndani ya Yesu.

Ukiona unataka kuomba then kushukuru kunajaza moyo wako dont rush just concentrate on that kushukuru kuna breakthrough kama hujui. Wana wa israel siku moja walifanya maandalizi ya kuimba na kusifu ila kabla ya kuanza walijikuta wakisema Mshukuruni Mungu kwa maana fadhili zake ni za milele. Those words invited breakthough to go before them, 2Nyak 20:21

Mshukuru Mungu unamaliza mwaka na kujiandaa kuingia mwaka mwingine.
Theme images by centauria. Powered by Blogger.