TUMIA MIFANO HII KUJIULIZA KAMA UNAELEWA UMUHIMU WA NAFASI ULIYO NAYO KATIKA KUMTUMIKIA MUNGU
Mfano wa OBADIA
4 kwa
kuwa ikawa, Yezebeli alipowaua manabii wa Bwana, Obadia akatwaa manabii mia, akawaficha hamsini hamsini katika pango,
akawalisha chakula na kuwapa maji).
12 Na itakuwa, mara mimi nikiondoka kwako, roho ya Bwana atakuchukua
uende nisikojua; nami nitakapokwenda kumwambia Ahabu, naye asipokuona, ataniua,
lakini mimi mtumishi wako namcha Bwana
tangu ujana wangu.
15 Eliya akasema, Kama Bwana wa majeshi aishivyo ambaye ninasimama
mbele zake, hakika nitajionyesha kwake leo.
1 Waf 18
Obadia
aliishi kwenye nyumba ya Yezebeli aliyekua amejaa uovu sana lakini alikua MCHA
MUNGU. Huu uchaji ndio ulimsukuma kuwaficha manabii wa Mungu saa Yezebeli
anataka kuwaua. Mungu alimpa ile nafasi ili aweze kujua siri zinazoendelea
ikulu juu ya watu wa Mungu. Kuna nafasi Mungu anakupa ili ukusanye data za
kusaidia watumishi wake. Usije ukafikiri Mungu akikuweka kuwa mkandalasi wa
wilaya hakuna analotaka ufanye kwa ajili yake. Nafasi yako ni ya muhimu kuliko
unavyo dhani katika kulitunza shauri la Mungu.
Ukiacha
kuitumikia iyo nafasi Mungu amekupa uwe na uhakika anao uwezo wa kukuondoa.
Kumbuka jinsi Mordekai alivyo mwambia Esta juu ya nafasi ya umalikia kwenye
nchio ya ugeni. Kama Esta angekaa kimya Mungu angewainulia msaada toka mahali
pengine kuwasaidia wayahudi.
Sasa huenda
nawe ni kama Esta, pamoja na kuwa na nafasi mahali fulani lakini hujui maana ya
iyo nafasi kwa jicho alilonalo Mungu. Kama Mordekai alimkumbusha Esta name
nakukumbusha kupitia somo ili, ukikaa kimya kwenye iyo nafasi Mungu atatumia
namna nyingine na kuachana na wewe.
Swali nataka
ujiulize
·
Kwa nini Obadia katika kujitetea ili Elisha aende kujionyesha
kwa Ahabu ilibidi neno “namcha Mungu tangu ujana wangu liandikwe”? Kulikua na
sababu gani ambalo uchaji ilikua lazima kuandikwa? Nini Mungu alitaka tujue
kuhusiana na uchaji?
7 Kumcha Bwana ni chanzo cha
maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.
Mith 1
Mith 1
6 Watu wangu wanaangamizwa
kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa
wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi
nami nitawasahau watoto wako.
Hosea 4
Nataka uone
hapo, sababu ya watu wa Mungu kuangamia inaonekana ni kukosa maarifa. Mtu
mchaji ana haya maarifa ambayo kimsingi pia yatamsaidia asiangamizwe. Ukisoma
Hosea ni kwamba asiye na maarifa yuko kwenye hatari ya kuangamizwa.
Obadia
kutokana na uchaji wake alikua na maarifa, na alijua kabisa kama akikubali kazi
aliyopewa na Eliya ya kwenda kumsimulia Ahabu kwamba walikutana na Ahabu
asimuone ndo ingekua mwisho wake na angeangamizwa. Sasa maarifa yalimsaidia
kupangua hoja ya Eliya na matokeo yake wakaenda wote kwa Ahabu.
Nataka uone
ukiwa unamtumikia Mungu unahitaji maarifa sio kawaida. Kuna watu utakutana nao
ambao utahitaji maarifa kupangua hoja zao vinginevyo watakutengenezea mitego
uangamizwe. Na wanaweza kuwa ni watu wa Mungu kama ilivyo kwa Eliya.
Sasa agano
jipya ngazi moja ya uchaji inaongezeka. Utakumbuka Matendo 10 kuhusu habari ya
Konelio. Huyu bwana alikua mchaji sana lakini hakuwa ameokoka. Uchaji utaji
utakusaidia utakua na mahusiano mazuri na Mungu lakini roho yako haiwezi kwenda
Mbinguni bila kumpokea Yesu. Konelio alihitaji atoe maisha yake kwa Yesu ili
uchaji wake uwe na maana zaidi. Kufuatana na biblia Yesu ni NJIA, KWELI na
Uzima mtu haendi kwa Baba ila kwa njia ya Yeye. Maana yake ni kwamba kama
hujampokea Yesu uchaji wako utakusaidia tu hapa duniani ila huna makao kwa Baba
mbinguni.
Mfano wa
NAAMAN
1 Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu
mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye
kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake Bwana alikuwa amewapa Washami kushinda;
tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma
2 Na
Washami walikuwa wametoka vikosi, wakachukua
mfungwa mmoja kijana mwanamke kutoka nchi ya Israeli; naye akamhudumia
mkewe Naamani.
3 Akamwambia bibi yake, Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule
nabii aliyeko Samaria! Maana angemponya ukoma wake.
15 Akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli; basi nakuomba upokee mbaraka kwa mtumwa wako.
15 Akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli; basi nakuomba upokee mbaraka kwa mtumwa wako.
2 Waf 5
Uwezo na
heshima aliyokuwa nayo Naamani ilitoka kwa Bwana. Lakini pamoja na kumpa iyo
heshima lakini alimuacha na ukoma kwenye mwili wake. Usije fikiri Mungu hayuko
kwa sababu ya tatizo unaloliona kwako lijaondolewa, Mungu anabaki kuwa Mungu
hata kama unafikiri hajakuondolea ilo tatizo lako.
Biblia haielezi wasifu wa huyu dada
aliyechukuliwa kama mateka toka Israeli ila tendo alilolifanya linatosha
kuonyesha huyu dada alitambua uwezo uliopo kwa Mungu vizuri ndio sababu alitoa
ushauri wa aina ile. Sio rahisi kwa house girl kutoa ushauri wa aina ile kwa
bosi wake kama hana uhakika nao. Nataka uone pamoja na nafasi ndogo sana
aliyokua nayo yule binti lakini hakukaa kimya na kuacha kuelezea habari za
Mungu wake. Nakumbusha tena, kwa nafsi yeyote uliyo nayo unaweza kulitumikia
kusudi la Mungu, kikubwa ni kwamba hapo ulipo usiache uchaji. Mazingira uliyo
nayo yasiondoe uchaji wako.
Jaribu kufikiri huyu mdada angejinyamazia nini kingetokea? Ni kweli Mungu aliacha ukoma kwenye mwili wa Naaman pamoja na kumpa heshima sana lakini ule ukoma Mungu aliuacha kama mtaji kwa ajili ya mtu mwingine kutambulika. Fikiri kama dada alsingetoa ushauri wa jinsi ile kama angeandikwa kwenye biblia.
Nafasi uliyo nayo Mungu anangoja uitumie kulitenda kusudi lake akutambulishe mbele za wengine, upige hatua moja zaidi. Ile nafasi dada alivyoitumia ndiyo iliyo mtambulisha Mungu wa Israel kwa Naaman. Pamoja na kwamba ni Mungu alimpa ile heshima ila Naamani hakuwa anamjua Mungu wa Israeli. Unaweza kukaa kimya ukifikiri ulio nao wanamjua Mungu kumbe hawamjui na Mungu amekuweka hapo ili umtambulishe kwao.
Jaribu kufikiri huyu mdada angejinyamazia nini kingetokea? Ni kweli Mungu aliacha ukoma kwenye mwili wa Naaman pamoja na kumpa heshima sana lakini ule ukoma Mungu aliuacha kama mtaji kwa ajili ya mtu mwingine kutambulika. Fikiri kama dada alsingetoa ushauri wa jinsi ile kama angeandikwa kwenye biblia.
Nafasi uliyo nayo Mungu anangoja uitumie kulitenda kusudi lake akutambulishe mbele za wengine, upige hatua moja zaidi. Ile nafasi dada alivyoitumia ndiyo iliyo mtambulisha Mungu wa Israel kwa Naaman. Pamoja na kwamba ni Mungu alimpa ile heshima ila Naamani hakuwa anamjua Mungu wa Israeli. Unaweza kukaa kimya ukifikiri ulio nao wanamjua Mungu kumbe hawamjui na Mungu amekuweka hapo ili umtambulishe kwao.
Mfano wa
VIJANA WASOMI KINA DANIEL
3
Mfalme akamwambia Ashpenazi, mkuu wa matowashi wake, awalete baadhi ya wana wa Israeli, wa uzao wa kifalme, na wa uzao
wa kiungwana;
4 vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu
kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena alimwambia
awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao.
Dan 1
“Awalete
baadhi” maana yake walikua wengi ila hakuwataka wote, kwa ivyo hao baadhi walio
patikana kwao ilikua ni zaidi ya bahati.
Lakini nataka
uone kosa kubwa ambalo Danieli hakulifanya kama ambavyo watu wengine wakipewa
nafasi Fulani huwa wanafanya ilo kosa. Ukisoma vizuri utaona udahili wa hao
vijana pia ulikua na lengo la kudahiliwa. Lengo la wao kudahiliwa ni ili
wasimamie kusudi la mfalme ila sio la Mungu. Ni rahisi sana mtu ukahajiliwa
mahali kisha ukasahau kwamba pamoja na kuwepo lengo la ofisi lakini lengo kubwa
la Mungu kukuweka hapo na sio kumweka mwingine ni ili wewe utunze kusudi lake
hapo. Fikiri kwamba kuna watu wengi mtaani wenye sifa kama za kwako lakini
hawako kwenye iyo ofisi na ujiulize ili swali kwa nini wewe?. Usije hata siku
moja kusingizia ofisi yako kuwa ndio imefanya ukose nafasi ya kumtumikia Mungu.
Ni sawa
kabisa unaweza kufikiri ukiwa shule lengo lako ni kusoma tu, lakini fikiri mara
mbili kwamba ni kweli hao ulio waacha mtaani na hawakupata nafasi ya kusoma
kweli Mungu hana mpango nao?. Utakuja ugundue huko kwenye nafasi uliyo nayo
only kwa ajili ya kusudi la Mungu Fulani ambalo huwezi kulitekeleza kama
ungekua nje na hapo shuleni.
Mambo ambayo
Danieli alikuaja kuyafanya kwenye sura ya pili na akuendelea ilimuhitaji kwanza
kuipata ile nafasi ya kudahiliwa kisha kumtumikia Mungu hata kwenye ile nafasi.