Header Ads

KUMPENDA BWANA MUNGU WAKO

 Marko 12:30-31
30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.
 31 Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.

Kumpenda Bwana MUNGU kwa moyo ni pale mtu unapoamua  Kuokoka na kumkili kwamba ni mwokozi wa maisha yako. Kumpenda kwa roho yako ni pale nafsi yako inapoamua kufanya kaz kwa kufuata maagizo ya MUNGU. Nafsi na moyo vyote uenenda sawa na MUNGU apendavyo.
Kumpenda Bwana kwa Akili zako ni pale unapoamua kuamisha Upendo wako kutoka kweny nafsi na mwili na kupeleka kwenye Akili na muda wote unawaza kumtumikia MUNGU na kutumia nguvu kuyatenda mapenz ya MUNGU

NAMNA YA KUMPENDA MUNGU WAKO
 Kufuata amri na maagizo ya MUNGU
Amri za MUNGU kwenye kutoka 20:1 zote zimemezwa na amri hii ya kumpenda Bwana MUNGU. Kwani ukimpenda MUNGU huwezi kuiba, kuzini, kuua ,kuwa na miungu mwingine
Swali
Jiulize leo unampenda MUNGU kweli au bado hujaamua? tafakari na uchukue hatua

Ameeen na MUNGU akubariki
Theme images by centauria. Powered by Blogger.