Header Ads

MUNGU ALITAKA TUJUE NINI KWA KUMTUMA EZEKIELI KWA WASIO SIKIA?


Swali linaulizwa na Jenipher kutoka Arusha mjini kuhusu utumishi wa Ezekieli

Kwanini Mungu alimtuma Ezekiel kwa Nyumba ya Israel,ilihali alijua tangu hapo kuwa Israel hatasikia? Ili ndio swali letu la msingi la leo kwenye mjadala tunaposoma hiki kitabu cha Ezekieli sura ya kwanza hadi ya nne.Swali likaendelea kupanuliwa:- Je Mungu alimpa Ezekiel ya kutaabika buree...!?? Nini hasa Kusudi la Huduma ya Ezekiel.......!!!!??

MAJIBU YA AWALI
Mtumishi Nickolaus kutoka Dsm akitoa majibu yake
1 Akaniambia, Mwanadamu, simama kwa miguu yako, nami nitasema nawe.
2 Naye aliposema nami, roho ikaniingia, ikanisimamisha; nikamsikia yeye aliyesema nami.
3 Akaniambia, Mwanadamu, nakutuma kwa wana wa Israeli, kwa mataifa wanaoasi, walioniasi mimi; wao na baba zao wamekosa juu yangu, naam, hata hivi leo.
4 Na wana hao wana nyuso zisizo na haya, na mioyo yao ni migumu. Mimi nakutuma kwa hao; nawe utawaambia, Bwana MUNGU asema hivi.
5 Nao, kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia, (maana ndio nyumba ya kuasi hao), hata hivyo watajua ya kuwa nabii amekuwako miongoni mwao
Eze 2

Mungu hata kama anajua.hutasikia  ila atafanya majukumu yake. Atafanya sehemu yake, Hata kama hutakuwa na Imani, Yeye Mungu atafanya part yake na part yake ni kukuletea Neno linalotakiwa kuweka Imani kwenye moyo wako.
Unajua Mungu ni Mwenye haki sana. Paulo anasema-Ukaonekane una haki Usimamapo Kuhukumu.
Mungu ameandaa siku ya Kutoa hukumu, lakini kwa jinsi alivyo mwenye Haki atahakikisha -kabla hajaileta Hukumu juu yako, anakuletea Neno. Na kwa Neno hilo, Utajua kuwa Mungu alisema na mimi..Hivyo kwenye Hukumu hutakuwa na Udhuru na Mungu ataonekana mwenye Haki.
Paulo anasema-Yote ya Mungu yaliyopaswa kufunuliwa yaliyokuwa yamefichwa tangu mwanzo yamefunuliwa kwa Kila mtu. Nakwambia Mungu ananjia ya kuhakikisha kila mtu juu ya nchi atamjua na kulisikia Neno la Kristo,,,ili kama hatasikia ajue kuwa hakika Yesu alinisemesha nami nikakataa.! Na atakapokuleta Hukumu, yeye ataonekana mwenye HAKI.
19 Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia.
20 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru;
Warumi 1.

Warumi 3.
3 Ni nini, basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je! Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu?
4 Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa, Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako,Ukashinde uingiapo katika hukumu.
Mungu is awesome sana -Haki ni sifa yake. Yaani kama utataka kujitetea siku anakuletea Hukumu -atataka Kuonekana mwenye Haki. Ndio Maana akamtuma Ezekiel kwa watu ambao alijua watakataa kusikia Neno. Ndio maana anaweza kukutuma leo na kesho kwa watu -na wakakataa kusikia Neno lako. Nawe usiseme taabu yangu na kazi yangu imekuwa bure. La hasha....!!! Unafanya Kutimiza Kusudi la Mungu.. Kuudhirisha Uweza wake, ili kuwafunga vinywa siku ya hukumu. Siku ya hukumu-utaona kuwa kumbe sikufanya kazi bure.
Kutokuitika kwa watu unapowaitia Wokovu, kusikufanye ukapunguza moto, ukaacha Kusudi la Mungu.  Piga Neno,wajue Alikuwako mtu wa Mungu katikati yetu.
19 Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu;
20 kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria
Warumi 3.
Nabii Ezekiel alienda kuwafunga Israel vinywa. Alienda kuwawekea Hukumu juu yao. Kama Vile leo hii -haki hii ambayo haipatikani kwa torati bali kwa Imani katika msalaba wa Yesu,, hivyo kila tuhubiripo Injili, tunaiweka hukumu ya Kristo juu ya ulimwengu na kuwafunga wanadamu vinywa.

16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.
19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu
Yohana 3.
Kama Yesu anavyosema -hakuja kuhukumu bali kuokoa -ila ukiangalia kwa sura nyingine ni kama amekuja kuiweka Hukumu juu ya wote ambao hawatamwamini. Kama Ezekiel-Walipolilataa, Hukumu ya Mungu iliwekwa juu yao kwa Neno la Ezekiel

Kujiunga na darasa letu kwa njia ya watsap tuma jina lako na namba kwenye email Graedybiblestudy@gmail.com
Theme images by centauria. Powered by Blogger.