KUMBUKA KUOMBA MAOMBI HAYA
Tar 11/02/2018
Neno la Kuongoza
1 Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana;
3 Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.
Ufu 1
Ufafanuzi
1. "hayana budi kuja upesi"
>>Kitabu cha ufunuo ni kati ya vitabu vilivyosema wazi kwamba uliyoyasoma yako karibu sana kutokea/hayana muda mrefu
2. "Heri, asomaye, ashikaye na asikiaye"
>>Kitabu cha ufunuo kinatoa Baraka kwa makundi matatu ya watu
Kuna Baraka za kusoma tu
Kuna Baraka za kusikia ulichokisoma
Kuna Baraka za kushika ulichosikia
MAOMBI
1. Ili kuepuka hatari ya kitakacho tokea upesi Mungu kwenye kila ujumbe amekua akisisitiza mtu kutubu. Nikupe mfano:- kwenye kanisa la Leodokia Ufu 3:14- ambalo ndilo tunaishi sasa amesema wazi kwamba Mtu vuguvugu atamtapika. Mtu yule ambaye ni mkristo lakini pia mzinzi. Ambaye ni mkristo lakini ni mpiga dili kazini.
>>Hujui upesi iyo ni lini, twende mbele za Mungu kwa toba kwa kila ujumbe alio achia kwenye hiki kitabu cha nyakati za mwisho
2. Omba Mungu akupe stamina ya kusoma, kuweza kusikia na ukisikia ushike.
Omba toba ikiwa ulikikatia tamaa kitabu hiki kisha mwambie Mungu akufundishe kwa upya kabisa...hata kama sisi tumefika mbali akupe stamina na kiu isiyo ya kawaida. Ni muhimu sana kuelewa hiki kitabu cha ufunuo mpenzi.
GBS JIFUNZE KWA KUANDIKA