USIKAE UKAZUBAA PIMA KILA ROHO, MAFUTA UNAYO NDANI YAKO
Tuanze kusoma maandiko yafuatayo:-
1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.
2 Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.
1 Yoh 4
Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote.
1 YOH. 2:20 SUV
Nyinyi, lakini, mlipata kumiminiwa Roho Mtakatifu na Kristo, na hivyo mnaujua ukweli.
1 Yohane 2:20 BHN
Lakini ninyi mmetiwa mafuta na yeye Aliye Mtakatifu, nanyi nyote mnaijua kweli.
1 Yohana 2:20 NEN
Mafuta tuliyopakwa na Aliye Mtakatifu, tafsiri nyingine inasema kumiminiwa Roho Mtakatifu na Kristo. Hivyo mafuta yanayozungumziwa hapa ni huyu Roho Mtakatifu tuliyemiminiwa pale tulipoamini. Changamoto ni kumiminiwa huyu Roho Mtakatifu, kwani wengine wanasema kuwa na Roho Mtakatifu inaambatana na udhihirisho wa kunena kwa lugha. Ukiwa nae huyu Roho Mtakatifu wewe unaijua kweli yote, tena unaujua ukweli hivyo unaweza kuugundua uongo.
Ukitaka kuenenda pasipo kuyumbishwa na elimu zilizo kinyume na kweli ya Kristo lazima uwe na Roho wake Kristo. Hawa jamaa wa mafunuo na mafuniko hawatakula pesa yako kabisa, kijanja janja hawawezi kujifaidia kwako. Hivyo, kwa kuwa unayo hayo mafuta, basi zijaribu kila roho, iliujue kama zinaenda sawa na kweli ya Kristo unayoifahamu ndani yako.
Ndio maana kunasehemu neno linasema, na amani iamue moyoni mwako, hapo ni kuangalia huyu Roho Mtakatifu ametulia kiasi gani ndani yako, na hii inategemea na kweli ya Kristo imefuatwa kwa kiasi gani. Soma NENO shika NENO
Na:- Kelvin Kidifu
GBS ARUSHA