UNAYO TABIA YA KUJIKUMBUSHA WEWE NI NANI?
Na: Madame Neema (Ney)
Bwana Yesu Asifiwe!
Mathayo 5:13-16
13 Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.
14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.
15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
Siku zote kumbuka kwamba wewe ni:-
- Chumvi ya dunia
- Nuru ya ulimwengu
Kuwa Nuru maana yake kila ufanyalo laonekana kwa wengine. Yesu asingetuita nuru ya ulimwengu kama Yeye asingekuwa nuru
12 Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
Yoh 8
Maana yake ni kwamba ili ubaki kuwa nuru ni jambo la msingi kung'ang'ana na Yesu kuhakikisha hakuna linalokutenga naye, kinyume na hapo ni ngumu kwako kuwa nuru. Ukitafakari jambo hili kumbuka kwamba we cannot live only to ourselves; we must have someone to shine to, and do so lovingly.
Dhana muhimu kwenye haya mambo mawili:- Chumvi na Nuru ni kwamba chumvi inahitajika kwa sababu ulimwengu unaoza na kuoza, na kama Ukristo wetu pia unaoza na kuoza, haitakuwa nzuri. Mwanga unahitajika kwa sababu dunia iko katika giza, na kama Ukristo wetu unaiga giza, hatuna chochote cha kuonyesha ulimwengu. Ili kuwa na ufanisi tunapaswa kutafuta na kuonyesha tofauti ya Kikristo. We can never affect the world for Jesus by becoming like the world.
Kujiunga na darasa letu la whatsap tuandikie +255758358236